Phone:
+2557 62 251 566

Physical address:
Dar-es Salaam, Tanzania

Dennis na Wimbi la Mabadiliko- kiswahili kitukuzwe

Today we are delving in the world of Swahili literature. When last did you read a Swahili novel also called Riwaya or Tamthilia ? We get to engage Dennis Shonko as a poet, writer and a mentor. Where it all started, He has authored many publications, been featured in many Kiswahili books and literal works.

This book is suitable for teens or young adults who would wish to immerse themselves in literature that shades light on societal democracy versus integrity . 

You may need a Kamusi to jog your memory :), but here at Minor Dtales, we promise to explore all forms of literature in the tapestry of culture and origin.

Ni nini kilikuchochea hadi ukaamua kuwa mwandishi?

Nilipenda sana kusikiliza utambaji hadithi redioni tangu nikiwa mdogo. Mno, nilipenda kusoma vitabu vya hadithi. Ndipo nami nikajiuliza siku moja, mbona nami nisijaribu kutumikisha Kiswahili changu kupitia uandishi? Ndipo nikaanza polepole kutunga hadithi hadi yakawa mazoea.

Ukiwa mdogo, ulipenda kusoma au kusikiliza kitabu kipi?

Nilivutiwa sana na Hekaya za Abunuwasi, Majuto ni Mjukuu na Manywele. Ni simulizi zilizokuwa na mvuto wa aina yake, sikwambii ucheshi! Michoro iliyokuwamo ilinivutia zaidi.

Ni ilhamu gani au kitu kipi hasa kilikufanya ufikiri ‘nataka kuwapa watu hadithi yangu’? 

Kama nilivyodokeza awali, nilifurahishwa na jinsi utambaji/usomaji hadithi unaweza kumuathiri mtu. Nilidhamiria kuiweka sawa jamii kupitia hadithi zangu. 

Pana chochote ulitamani kujua kabla ya kuanza?

Mmm, la! Nilipoanzia safari hii ni Mungu kupenda. Ya kale hayanihangaishi!

Je, uliandika hadithi ipi ya kwanza kabisa na ilihusu nini?

Niliita “Harusi ya Paka na Panya”. Ni hadithi iliyosimulia namna wanyama walilenga kujenga uhusiano mwema kati yao. Hilo lilitokana uhasama uliokuwa ukizuka kila palipotokea ukame—wanyama walimalizana wenyewe ili kupata chakula. Basi yalipozidi, wakaamua ili uhasama uishe, na kama ishara ya maamuzi yao, lazima Paka na Panya wangeoana. Ikawaje sasa? Hayo ni ya siku nyingine kwani kazi yenyewe haijachapishwa kufikia sasa!

Malizia sentensi: Ili kujenga ubunifu wangu, mimi hupenda kusikiliza zaidi badala ya kuzungumza.

Ni vitabu au waandishi gani waliokupa msukumo wa kuandika au kuanza safari ya ubunifu?

Waandishi na kazi zao ni wengi tu. Kutaja tu wachache: Hayati Prof. Ken Walibora, Mhadhiri Henry Indindi, Said A. Mohamed, Bi. Pauline Kea, Bi. Clara Momanyi, Prof. K.W Wamitila. Wamenilea kwa njia ya moja kwa moja au kupitia kazi zao. 

Je, wewe hufanya nini wakati hauandiki?

Kusoma vitabu au kutazama filamu.

Kwa wanaosikia kuhusu kitabu chako kwa mara ya kwanza, wape muhtasari wa kitabu chenyewe.

Kitabu cha Mwisho wa Siri ni novela ya kusisimua kuhusu watoto wanaokumbana na changamoto mbalimbali kipindi cha uchaguzi nchini. Jairo na Katitiro wana mitazamo tofauti kuhusu utoaji hongo nyakati za uchaguzi. Ni mvutano unaotishia uhusiano kati yao wenyewe na wa wazazi wao. Maadili yanawekwa katika mizani kuanzia mwanzo hadi mwisho! Haiwi kazi rahisi kwa watoto kukosoa matendo maovu ya wakubwa wao, ikikumbukwa kuwa jamii humtaka mtoto kutenda anayoshurutishwa kufanya na waliomzidi umri. Hata hivyo, penye nia njema, wema na mema hushinda! 

You can find more of Dennis Shonko’s on his platform : CLICK HERE 


6 Comments

  1. Quite the refresher course in Kiswahili!
    Good one!
    Penye nia njema, wema na mema hushinda❤️

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Select your currency
KES Kenyan shilling